• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapeleka kundi la tatu la wataalam wa afya nchini Italia

    (GMT+08:00) 2020-03-25 18:30:47

    Wataalum 14 wa afya kutoka mkoa wa Fujian, China wamewasili nchini Italia kuisaidia nchi hiyo kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona (COVID-19).

    Majukumu ya wataalam hao ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa kuzuia na kudhibiti maambukizi hayo na kutoa mapendekezo ya matibabu kwa hospitali na wataalam wa afya nchini humo.

    Wataalum hao pia wamepeleka tani 8 za vifaa vya matibabu vilivyotolewa na mkoa huo kwa Italia, ikiwemo nguo elfu 3 za kujikinga na virusi, mask laki 3 za kiudaktari, mask elfu 20 za aina ya N95 na mask elfu 3 za kufunika uso mzima.

    Awali, China ilituma vikosi viwili vyenye madaktari 22 na tani 20 za vifaa vya matibabu kusaidia Italia kupambana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako