• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Yanga salama salmini

  (GMT+08:00) 2020-03-25 18:30:58

  Uongozi wa Klabu ya Yanga, umewataka wanachama na wadau wake, kupuuza taarifa zinazosambazwa na mmoja wa wanachama wao, kuwa mdhamini wa timu hiyo, Kampuni ya GSM ina mpango ya kuikacha. Taarifa ya GSM kujitoa kuidhamini Yanga, ilisambaa juzi, ikidaiwa hatua hiyo inatokana yaliyojiri katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo na wadhamini hao. Baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo, uongozi wa Yanga kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli, jana ulijitokeza na kukanusha kuwapo kwa mpango wa GSM kujiondoa kuwadhamini. Bumbuli alisema hakuna mgogoro wowote kati ya klabu yao na GSM, hivyo taarifa zinazoenezwa ni uzushi wenye lengo baya na maendeleo yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako