• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: UAF yapunguza ratiba ya mashindano ya riadha kwa mwaka huu

  (GMT+08:00) 2020-03-25 18:31:17

  Shirikisho la Riadha nchini Uganda (UAF) limefuta shindano moja kutoka kwenye ratiba yake ya mwaka na kubadilisha mashindano mengine ikiwa ni kufanyia marekebisho mashindano yaliyofutwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona. Msemaji wa Shirikisho hilo Namayo Mawerere amesema, uamuzi huo unaendana na marufuku ya mwezi mmoja iliyowekwa na serikali inayozuia shughuli zote za michezo. Mashindano mengine yote ya kikanda yamepangwa kufanyika Mei 30 katika sehemu zilizotangazwa awali, isipokuwa Mashindano ya Kanda ya Mashariki ambayo yatafanyika Soroti badala ya Tororo kama ilivyopangwa awali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako