• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Chris Kirubi kununua asilimia 20 ya hisa katika Kampuni ya Uwekezaji ya Centum

  (GMT+08:00) 2020-03-25 19:39:46

  Mwekezaji Chris Kirubi nchini Kenya amesema yuko tayari kununua asilimia 20 ya hisa katika Kampuni ya Uwekezaji ya Centum za thamani ya shilingi 2.7 bilioni (dola milioni 27).

  Huu utakuwa ununuzi wa mkubwa wa pili kwa Bwana Kirubi, na anasema kuwa bei ya hisa ya kampuni hiyo kwenye Soko la Nairobi (NSE) inaendelea kupuuzwa.

  Mfanyabiashara huyo alitumia zaidi ya shilingi bilioni 1 (dola milioni 10) kati ya Septemba 2013 na Agosti 2015 ili kuinua hisa zake katika kampuni hiyo kutoka asilimia 24.99 iliyopita hadi asilimia 30 ya sasa.

  Tangazo la ununuzi mpya wa hisa linakuja baada ya hisa za Centum kushuka zaidi kwa kipindi cha miaka saba na kufikia shilingi 20.25 hiyo ikiwa inaashiria kupungua kwa asilimia 35 katika miezi 12 pekee.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako