• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Serikali kuajiri 610 madaktari

  (GMT+08:00) 2020-03-25 19:40:30

  Serikali ya Tanzania imetangaza ajira za madaktari 610 ili kujaza nafasi kwenye hospitali za Halmashauri na vituo vya afya nchini.

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Nyamhanga, amsema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa Februari mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Madaktari Duniani, ya kutoa ajira mpya kwa madaktari 1,000 nchini.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Nyamhanga, madaktari watakaoajiriwa ni wa binadamu na meno waliohitimu katika vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako