• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mauzo ya Nike yaongezeka China

  (GMT+08:00) 2020-03-25 19:41:01

  Kampuni ya mavazi ya michezo Nike imesema mauzo ya mtandaoni yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 nchini China .

  Kampuni hiyo imefunga duka zake nyingi ulimwenguni, lakini inasemaa asilimia 80 ya maduka yake nchini China sasa yamefunguliwa tena.

  Mkurungezi mtendaji mkuu wa Nike John Donahoe hata hivyo amesema wiki kadhaa zijazo zinaweza kuwa kipindi kigumu.

  Amesema anatumai kuwa Nike inaweza kujifunza kutoka China ili kusaidia utendaji wa masoko ya Magharibi.

  Nike iliripoti kushuka kwa mauzo kwa asilimia 5 nchini China hadi dola bilioni 1.5 katika robo yake ya mwisho ya mwaka wao ya kifedha.

  Hata hivyo sasa inategemea soko hilo kulinda maduka ambayo yameathirika hasa nchi za magharibi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako