• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yapitisha mpango wa kutoa dola trilioni 2

    (GMT+08:00) 2020-03-25 19:41:24

    Viongozi wa Ikulu ya Marekani na wa Seneti wamekubaliana Jumatano kuhusu mpango mkubwa wa serikali kutoa dola trilioni 2 kusaidia uchumi wakati huu nchi hiyo ikipambana na virusi vya Corona.

    Seneti imekuwa ikijadili mpango huo kwa siku kadhaa ambao hatua ya gharama kubwa katika historia ya Congress.

    Mkurugenzi wa maswala ya sheria wa Ikulu Eric Ueland alitangaza makubaliano hayo akiyataja kufikiwa baada ya siku za majadiliano makali .

    Maelezo kamili bado hayajatolewa lakini zaidi ya masaa 24 iliyopita, kumekuwa na mapendekezo kadhaa kama vile dola bilioni 250 zimetengwa kwa malipo ya moja kwa moja kwa watu na familia, dola bilioni 350 kuwa mikopo kwa biashara ndogo ndogo na dola bilioni 250 kwa sekta ya bima.

    Chini ya mpango huo unaojadiliwa, watu wanaopata mshahara wa dola 75,000 kwa mwaka watapokea dola 1,200 huku nao wana ndoa wakipata 2,500 na dola 500 kwa kila mtoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako