• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuwepo kwa umoja, ushirikiano na uratibu duniani katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-25 20:16:47

    Rais Xi Jinping wa China kesho atahudhuria mkutano maalum wa viongozi wa kundi la G20 kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona utakaofanyika kwa njia ya video.

    Akieleza matarajio ya China ya mkutano huo, naibu waziri wa mambo ya nje wa China Ma Zhaoxu amesema, chini ya uongozi wa rais Xi Jinping, China imefanikiwa kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo. Amesema rais Xi kuhudhuria mkutano huo kumeonesha nia thabiti ya China kushirikiana na jamii ya kimataifa kukabiliana na virusi hivyo, pamoja na mtazamo wake wa kuunga mkono kundi la G20 kuongeza uratibu na ushirikiano katika kutuliza uchumi wa dunia.

    Ma amesema, nchi wanachama wa kundi la G20 wanatakiwa kuongeza umoja na kutoa ishara yenye nguvu ya kukabiliana na changamoto kwa pamoja na kuinua imani ya jamii ya kimataifa. Ma ameahidi kuwa mbali na kukabiliana vizuri na maambukizi hayo ndani ya nchi, China itaendelea kutoa msaada kwa nchi zinazoathiriwa zaidi na maambukizi hayo. Pia ametoa wito kwa wanachama wa kundi hilo kuimarisha uratibu kuhusu sera za uchumi, kufungua mlango wa masoko, na kuhakikisha uwazi, utulivu, na usalama wa mlolongo wa uzalishaji bidhaa duniani ili kukabiliana na athari mbaya zinazotokana na maambukizi hayo kwa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako