• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: Wanunuzi wa tiketi za Olimpiki kujua hatma yao baadaye

    (GMT+08:00) 2020-03-26 09:41:57

    Wanunuzi wa tiketi ya michezo ya Olimpiki 2020 iliyopangwa kufanyika mjini Tokyo nchini Japan kuanzia Julai 24 hadi Agosti 9, watafahamu wiki chache zijazo iwapo itawezekana kutumia tiketi hizo baada ya mashindano hayo kuahirishwa hadi mwaka 2021. Wateja wengi walionunua tiketi hizi wakiwemo maelfu ya Wakenya, wamekuwa na hamu kubwa kufahamu iwapo tiketi hizo zitatumika ama wataishia kupoteza fedha zao kutokana na hatua ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) na waandaaji Japan kuamua kuisukuma mbele kwa sababu ya hofu ya virusi hatari vya corona, ambavyo vimeua karibu watu 20, 000 kote duniani. Wanamichezo 87 wa Kenya wamefuzu kushiriki michezo hiyo wakitoka katika fani mbalimbali zikiwezo raga ya wachezaji saba kila upande wanawake na wanaume, wanamasumbwi wawili mwanamume na mwanamke, taekwondo, uogeleaji na timu ya riadha ya wanaume na wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako