• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CORONA: Mwanariadha wa Kenya aliyekataa kujiweka karantini atiwa mbaroni

  (GMT+08:00) 2020-03-26 09:42:13

  Mwanariadha kutoka Eldoret amewekwa karantini kwa lazima katika Taasisi ya Mafunzo ya Viwanda nchini Kenya baada ya kukamatwa ndani ya matatu katika barabara ya Nakuru-Eldoret. Samson Ruto alirejea nchini Kenya akitokea Ufaransa kupitia India na Ethiopia Jumapili, Machi 22 na alikuwa akisafiri kuelekea Eldoret akitumia usafiri wa umma. Baada ya polisi kupokea habari kuhusu mwanariadha huyo waliiwekea matatu hiyo kizuizi katika eneo la Kibunjia na kumkamata mwanariadha huyo kabla ya kumsafirisha hadi kwenye taasisi hiyo. Mwanariadha huyo alikuwa akizungumza kwenye simu kuhusiana na ziara yake ughaibuni wakati abiria wengine waliokuwa katika Matatu hiyo walimsikia na kuwajulisha polisi. Ruto alifichua kwamba alisafiri hadi Ufaransa kushiriki shindano ambalo baadaye liliahirishwa kutokana na janga la homa ya corona na ndipo akalazimika kuelekea India kwa shindano lingine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako