• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MASUMBWI: Pambano la tatu kati ya Tyson Fury na Deontay Wilder kufanyika Oktoba

  (GMT+08:00) 2020-03-26 09:42:55

  Promota Frank Warren amesema bingwa wa dunia wa heavyweight Muingereza Tyson Fury anaweza kupigana na Mmarekani Deontay Wilder katika pambano lao la tatu mwezi Oktoba. Mwezi uliopita Fury, mwenye miaka 31 alimtwanga Wilder kwa KO katika raundi ya saba katika ukumbi wa MGM Grand huko Las Vegas na kuondoka na mkanda wa WBC. Hata hivyo kabla ya hapo, Disemba 2018 walipigana katika pambano lao la awali huko Los Angeles na kuishia sare iliyogubikwa na utata mkubwa. Sambamba na hilo Joshua naye sasa amepangiwa kupambana na Mbulgaria Kubrat Pulev katika uwanja wa Tottenham Hotspur Juni 20, ingawa promota wa Joshua, Eddie Hearn, amesema siku ya pambano inaweza kusogezwa mbele hadi Julai kwasababu ya msimu wa Ligi ya Premier huenda ukachelewa kumalizika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako