• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda yasitisha usafiri wa umma kwa siku 14 ili kuzuia kuenea kwa COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-03-26 10:56:17

  Rais Yoweri Museveni wa Uganda jana Jumatano alitangaza kusitisha usafiri wa umma kwa siku 14, ikiwa ni moja ya hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona nchini humo.

  Rais Museveni amesema vyombo vyote vya usafiri wa umma ikiwemo teksi, mabasi, treni na pikipiki (Bodaboda), vinatakiwa kusitisha huduma. Magari binafsi yanaruhusiwa kusafiri isipokuwa yanatakiwa kubeba watu wasiozidi watatu akiwemo dereva. Ameongeza kuwa magari ya mizigo, magari ya wagonjwa na yale ya huduma za usalama yanaruhusiwa kusafiri.

  Rais Museveni pia ameagiza kuwa masoko yote nchini humo yanaruhusiwa kuuza vyakula tu.

  Kabla ya hapo, Uganda ilifunga mipaka yake na kupiga marufuku mikusanyiko yote ya umma, kufunga shule na sehemu za ibada. Mpaka sasa Uganda imethibitisha maambukizi 14 ya virusi vya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako