• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe aushukuru Mfuko wa Jack Ma wa China kwa msaada wake

  (GMT+08:00) 2020-03-26 10:56:33

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ameushukuru Mfuko wa Jack Ma wa China kwa kuchangia vifaa vinavyohitajika kupambana na COVID-19 kwa nchi hiyo.

  Zimbabwe, ambayo imerekodi maambukizi matatu ya virusi vya Corona, Jumanne ilipokea shehena ya vifaa vya kimatibabu ikiwemo vitendanishi vya upimaji, maski na nguo za kujikinga, ikiwa ni sehemu ya msaada wa China kwa Afrika.

  Rais Mnangawa amesema hiki ni kitendo cha urafiki wa kweli ambacho ni muhimu katika kuwasaidia kupambana na virusi vya Corona.

  Wakati huohuo, Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe imetangaza kusitisha shughuli zote za uchaguzi ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, ambao umesababisha kifo cha mtu mmoja nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako