• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Tanzania yafikia 13

  (GMT+08:00) 2020-03-26 10:57:09

  Waziri wa afya wa Zanzibar, Tanzania Bw. Hamad Rashid amethibitisha mtu wa pili aliyeambukiziwa virusi vya Corona visiwani Zanzibar, na kufanya idadi ya watu walioambukizwa nchini Tanzania kufikia 13.

  Bw. Rashid amesema mgonjwa huyo mwanamke ni raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 mke wa raia wa Ghana, ambaye alithibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona wiki iliyopita. Watu hao wawili wametengwa kwa uchunguzi wa kiafya na kupewa matibabu, ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

  Ameongeza kuwa mtu mmoja anayedhaniwa kuambukizwa virusi vya Corona amewekwa karantini kwenye kisiwa cha Pemba. Hadi sasa watu 65 wamewekwa kwenye karantini kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya kwa siku 14 huko Zanzibar.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako