Wizara ya kilimo ya Kenya imetangaza mipango ya kuongeza idadi ya ndege zinazotumiwa kunyunyiza dawa za kuulia nzige wa jangwani kutoka 9 hadi 20.
Waziri wa kilimo, mifugo, uvuvi na ushirika wa Kenya Bw. Peter Munya amesema kutokana na madhara waliyoyaona hadi sasa, kuna haja ya kuweka ndege 10 za kunyunyiza dawa na 10 kwa ajili ya uchunguzi.
Bw. Munya amesema katika miezi mitatu iliyopita, nzige wameharibu mashamba mengi na kutishia usalama wa chakula nchini Kenya, akiongeza kuwa serikali pia inakusudia kupata magari 20 yenye vifaa vya kunyunyizia dawa ardhini, na kutoa mafunzo kwa wahudumu 500 na maofisa ugani 240, na kuwapa zana na kuwatuma kwenye maeneo yaliyoathirika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |