• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkuu wa WTO atahadharisha kuhusu kuporomoka kwa biashara, na kutoa wito kwa suluhisho la dunia dhidi ya COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-03-26 10:57:48

  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la biashara duniani (WTO) Bw. Roberto Azevedo ametahadharisha kuhusu kuporomoka kwa biashara duniani, na kutoa wito kutafuta suluhisho la dunia ili kutatua changamoto zinazoikabili dunia nzima kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.

  Katika ujumbe kwa njia ya video uliotolewa na WTO, Bw. Azevedo amekiri kwamba virusi vya Corona vitakuwa na athari kubwa kwa uchumi, biashara, na haswa nafasi za kazi na maslahi ya watu, akiongeza kuwa makadirio ya hivi karibuni kuhusu kushuka kwa uchumi na kupotea kwa nafasi za ajira ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa wakati wa msukosuko wa kifedha uliotokea miaka kadhaa iliyopita, na WTO itatoa makadirio kuhusu biashara wiki chache zijazo.

  Pia ametahadharisha kuwa wachumi wanaweza kukadiria kuporomoka kwa biashara, na kusisitiza umuhimu wa uwazi kuhusu hatua zinazohusiana na biashara, hivyo itakuwa hatua muhimu kwa nchi nyingi zinazotegemea vifaa vya matibabu vinavyoagizwa kutoka nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako