• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China azungumza na chansela wa Ujerumani kwa njia ya simu

  (GMT+08:00) 2020-03-26 10:59:13

  Rais Xi Jinping wa China jana usiku alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel.

  Rais Xi amesisitiza kuwa China inaiunga mkono Ujerumani kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, pia inapenda kutoa msaada kwa Ujerumani kadiri iwezavyo, na inapenda kubadilishana uzoefu na Ujerumani kuhusu kinga na tiba ya COVID-19, na kuimarisha ushirikiano kati yao kwenye utafiti wa chanjo na dawa.

  Bibi Angela Merkel amesema Ujerumani inapenda kufanya ushirikiano na China kwenye utafiti wa chanjo na dawa, na kuweka mfano wa mshikamano dhidi ya COVID-19.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako