• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO yazitaka nchi mbalimbali zisipoteze kipindi cha fursa ya pili dhidi ya COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-03-26 10:59:33

  Mkurugenzi wa Shirika la afya duniani (WHO) Dr. Tedros Ghebreyesus jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amezitaka nchi mbalimbali zisipoteze kipindi cha fursa ya pili cha kuzuia kuenea kwa COVID-19.

  Dk. Tedros amesema miezi miwili iliyopita, alikuwa anasisitiza kuwa virusi vya Corona ni "adui mkubwa zaidi wa umma", lakini nchi nyingi hazikufanya maandalizi na kuchukua hatua za lazima katika muda huo mrefu, na kupoteza kipindi cha fursa ya kwanza cha kuzuia mlipuko wa virusi hivyo. Amesema baada ya kuenea duniani kwa virusi hivyo, nchi nyingi zimechukua hatua za kufunga shule na viwanda, kufuta michuano, na kuwataka raia wakae nyumbani, hatua hizo zenyewe haziwezi kuondoa virusi, lakini zimetupatia fursa ya pili kuzuia virusi hivyo.

  Amezitaka nchi mbalimbali zisipoteze tena fursa ya pili, na kuchukua hatua za kuwatafuta, kuwapima, kuwaweka karantini, kuwafuatilia, na kuwatibu watu walioambukizwa COVID-19 kwenye kipindi hicho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako