• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Guardiola achangia bilioni 2 kupambana na Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-26 17:16:31

  Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amechanga pauni 920,000 sawa na Sh. Bilioni 2.5 za Tanzania kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona nchini Hispania. Kocha huyo ambaye kwa sasa yuko jijini Barcelona, amekutana na wanasheria wake ili kujua njia nzuri ya kutumia fedha hizo. Inasemekana fedha hizo zitakwenda kwenye kampeni ya kupambana na virusi vya Corona inayofanywa na Chuo cha Madawa cha Barcelona na Taasisi ya Misaada ya Angel Solar Daniel. Hispania ni nchi iliyoathirika zaidi na maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo mpaka jana, jumla ya watu 49,400 walithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako