• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Wanariadha waijia juu RT

  (GMT+08:00) 2020-03-26 17:17:57

  Wanariadha maarufu mkoani Arusha, Tanzania, wamesema viongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) ni batili na wamevunja katiba ya Shirikisho hilo. Kufuatia hali hiyo, wanariadha hao wameliomba Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuvunja uongozi huo na kuunda kamati ya muda itakayowashirikisha wanariadha, lengo likiwa ni kutaka ushirikishwaji wa pamoja kwa maslahi ya mchezo huo. Mwanariadha mkongwe Shenya Imori amesema, hivi karibuni, BMT iliunda Kamati ya Muda kufanya marekebisho ya Katiba ya Shirikisho hilo, kitu ambacho ni kama kiini macho, kwani kamati hiyo inapaswa kushirikisha wanariadha, ambao ndio wavuja jasho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako