• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Morrison afunguka alichozungumza na Simba

  (GMT+08:00) 2020-03-26 17:19:02

  Mshambuliaji nyota wa Yanga, Bernard Morrison amekiri mwenyewe kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na mazungumzo kwa ajili ya kujiunga na Simba. Morrison amesema Simba walimfuata tayari akiwa na mkataba na Yanga wakitaka ajiunge nao na mazungumzo kwa asilimia kubwa yalifanywa na wakala wake. Raia huyo wa Ghana ambaye tangu ametua nchini ameifungia Yanga mabao matatu, amesema Simba walitumia nafasi ya kumshawishi kujiunga nao baada ya kugundua ana mkataba wa miezi sita tu na klabu ya Yanga. Tayari Morrison amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga na kwanza amekuwa akitumia muda wake mwingi kufanya mazoezi binafsi nyumbani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako