• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: ZFF yakumbusha msisitizo Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-26 17:21:06

  Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) limewataka wachezaji, viongozi, mashabiki, na wadau wa mcezo huo visiwani humo kutoa kauli na machapisho mbalimbali juu ya kujikinga na virusi vya Corona. Katibu Mkuu wa ZFF, Mohamed Ali Hilali amesema ugonjwa huo ni janga la kimataifa na kamwe halipaswi kudharauliwa kama baadhi ya wananchi wanavyofanya. Hilali amesema ZFF inaendelea kuungana na serikali kwa kuzifanyia kazi kauli na maagizo yote yanayotolewa na Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed katika kupambana na virusi vya Corona. Amesema hayo baada ya baadhi ya watu na taasisi kuendelea kucheza mechi za kirafiki katika maeneo ya mashambani Unguja na Pemba wakiamini kuwa huko hakuna maambukizi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako