• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa msaada kwa nchi 89 kukabiliana na virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-26 18:24:16

  Naibu mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la China Bw. Deng Boqing amesema, China imetoa msaada kwa nchi 89 na mashirika manne ya kimataifa ili kukabiliana na virusi vya Corona, na duru mpya ya mipango ya utekelezaji wa msaada inaandaliwa.

  Deng amesema msaada huo wa kibinadamu wa dharura kwa nchi za nje ni operesheni inayotekelezwa ndani ya muda mfupi zaidi na kwa eneo kubwa zaidi tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949.

  Ameeleza kuwa wafanyakazi wa afya wa China na vifaa vya matibabu vimepelekwa kwa nchi 28 za Asia, 16 za Ulaya, 26 za Afrika, tisa za Amerika na 10 za Pasifiki Kusini. Amesema, katika msingi wa kudhibiti ipasavyo maambukizi nchini, China imetunga mpango wake wa msaada kwa mwafaka na kutoa msaada kwa nchi nyingine kutokana na uwezo wake.

  Akizungumzia hatari inayozidi kuikabili China kutokana na kesi za virusi vya corona za watu waliosafiri kutoka nje, Deng amesema msaada wa China kwa nchi nyingine pia unachangia juhudi za jamii ya kimataifa katika kukabiliana na virusi hivyo, na kuimarisha mafanikio yaliyopatikana kwa jasho kubwa katika kuzuia kuenea kwa virusi hivyo nchini China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako