• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano wa kimataifa wafanyika katika kutafiti chanjo ya Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-26 18:24:43

  China imeimarisha ushirikiano katika kutafiti na kuendeleza chanjo dhidi ya virusi vya corona.

  Naibu waziri wa sayansi na teknolojia Xu Nanping amesema chanjo ni muhimu katika kupambana na ugonjwa huo unaoikabili dunia nzima, na ni uamuzi sahihi kuwa na ushirikiano wa kimataifa wakati kazi za kutafiti na kuendeleza chanjo ni ngumu na zinakabiliwa na sintofahamu nyingi. Xu pia amesema China ilitangaza hadharani mpangilio kamili wa vinasaba vya virusi vya Corona muda mfupi baada ya kuugundua, na inatarajia kuwa nchi mbalimbali zitaweza kuanza kutafiti na kuendeleza chanjo mapema.

  China imetekeleza kwa pamoja mbinu 5 za kiteknolojia katika kutafiti chanjo, na moja kati yao ilianza kufanyiwa majaribio kwa binadamu Machi 16. Xu amesema mbinu hizo zote ziko wazi kwa ushirikiano wa kimataifa, ambao unaendelea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako