• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China ajibu barua ya mkurugenzi mkuu wa WHO

  (GMT+08:00) 2020-03-26 18:55:10

  Rais Xi Jinping wa China amejibu barua ya Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Tedros Ghebreyesus, akimpongeza kwa juhudi zake katika kuhimiza mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani, na kusema China itaendelea kuiunga mkono jumuiya ya kimataifa katika kazi hiyo.

  Rais Xi amesema, kwa sasa hali ya kinga na udhibiti wa mambukizi ya virusi vya Corona imekuwa nzuri nchini China, na utaratibu wa uzalishaji na maisha unaendelea kurudi katika hali ya kawaida. Amesema China inafuatilia hali ya kinga na udhibiti wa ugonjwa huo ndani na nje ya nchi na hali ya uchumi duniani, kubadilisha kipaumbele kwa kazi na hatua za kukabiliana, ili kuhakikisha ushindi wa vita dhidi ya maambukizi hayo.

  Rais Xi amesisitiza kuwa, maambukizi ya virusi vya Corona yamethibitisha kwa mara nyingine tena kuwa binadamu ni jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, hivyo jamii ya kimataifa inapaswa kusaidiana na kushirikiana. Ameongeza kuwa, China inapenda kushirikiana na WHO na nchi nyingine kutoa mchango kwa ajili ya kulinda usalama wa afya ya umma duniani.

  Tarehe 17 mwezi huu, Bw. Tedros alimwandikia barua rais Xi kupongeza juhudi kubwa za China katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako