• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Konokono wavamia mashamba ya mchele Mwea,Kenya

    (GMT+08:00) 2020-03-26 19:31:11

    Wadudu aina ya konokono wamevamia mashamba ya mchele katika mradi wa umwagiliaji wa Mwea,nchini Kenya.

    Konokono hao wamesababisha hasara kubwa na wakuylima wanahofia huenda wadudu hao wakaharibu kabisa mimea ambayo walipanda hivi majuzi.

    Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na uvamizi wa wadudu hao ni Thiba,Kiorugari,Nguka,Kimbimbi,Murubara na Mathangauta.

    Wakulima wanasema kuna uhaba wa mchele nchini hivi sasa ,na huenda hali ikawa mbaya zaidi iwapo hatua za kuwaangamiza hazitachukuliwa.

    Mwea ndio eneo linalokuza mchele kwa wingi nchini Kenya,na eneo hilo hutoa asilimia 80 ya mchele wote unaokuzwa nchini humo.

    Mradi wa Mwea ni wa ekari 30,350 ambapo ekari 22,000 zinakuzwa mchele huku zilizosalia zikitumiwa kwa makazi na kilimo cha mazao mengine ya chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako