• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania-Waziri wa Viwanda Innocent Bashungwa aagiza uzalishaji zaidi wa vitakasa mikono

  (GMT+08:00) 2020-03-26 19:31:55

  WAZIRI wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Innocent Bashungwa, jana alikutana na wazalishaji wa vitakasa mikono (sanitizer) ili kuweka mikakati ya pamoja na kuongeza uzalishaji kutokana na tishio la ugonjwa wa corona.

  Akifungua kikao hicho, Bashungwa alisema chimbuko la kikao hicho ni kutokana na ziara aliyoifanya kwenye maduka na viwanda vinavyotengeneza bidhaa hiyo na kubaini kuwapo uhaba wa vitakasa hivyo.

  Alisema kikao hicho kitatoka na mikakati ya kupambana na ugonjwa huo kwa kuhakikisha vitakasa hivyo vinazalishwa kwa wingi na kukidhi mahitaji.

  Alisema kupambana na corona kunahitaji ushirikiano wa pamoja na serikali, hivyo ni lazima waangalie serikali itimize majukumu yapi na wazalishaji watimize wajibu gani.

  Alisema lengo ni kuhakikisha uzalishaji unaongezwa na kupatikana kwenye maeneo yote nchini humo na kwa wingi kutaondoa kero ya bei.

  Aidha alisema alishaagiza Tume ya Ushindani (FCC) na Shirika la Viwango nchini Tanzania (TBS), kufanya msako nchi nzima ili kuwachukulia hatua wanaotaka kujitajirisha kwa mgongo wa Watanzania.

  Bashungwa alisema linatakiwa kuwapo soko huria la kuangalia utu na si kuwakomoa watu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako