Rais wa Uganda Yoweri Museveni jumatano jioni alipiga marufukua matumizi ya ya usafiri wa umma kwa muda wa siku 14 mara moja.
Wakati akihutubia taifa jana,Rais Museveni alisema kwamba katika hatua za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona, usafiri wote wa umma umepigwa marufuku.Hii ni pamoja na teksi,daladala,mabasitreni za bairia,bodaboda.
Alisema ni magari ya kibinafsi tu yatakayoruhusiwa barabarani,na magari hayo yataruhusiwa kubeba abiria watatu tu.
Aidha Museveni alisema magari mengine yatakayoruhusiwa barabarani ni malori yanayobeba chakula.
Rais huyo pia alipiga marufuku maduka na masoko yasiyouza chakula kwa muda usioijulikana.
Kufikia jumatano Uganda ilikuwa na visa 14 vya wagonjwa wa corona.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |