Rais Xi Jinping wa China amesema China itaongeza nguvu ya kutoa malighafi ya dawa, mahitaji ya kila siku na vifaa vinavyohusu mapambano dhidi ya virusi vya corona kwa masoko ya kimataifa, pia itaendelea kutekeleza sera zenye nguvu na utulivu za mambo ya fedha. China pia itashikilia sera ya kufungua mlango kwa nje, kuongeza maeneo yanayoweza kuwekezwa na nchi za nje, kuendelea kuboresha mazingira ya kibiashara, kuzidi kuagiza bidhaa kutoka nje, na kuchangia utulivu wa uchumi wa dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |