• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la G20 yaingiza dola za kimarekani trilioni 5 katika uchumi wa dunia ili kukabiliana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-27 10:57:40

    Kundi la G20 limetangaza kuwa litachukua hatua za haraka na madhubuti, pamoja na kuingiza dola za kimarekani zaidi ya trilioni 5 katika uchumi wa dunia, ikiwa ni sehemu ya sera inayolengwa ya kifedha, hatua za kiuchumi na mipango ya uhakikisho ya kumaliza athari za kijamii, kiuchumi na kifedha kutokana na virusi vya Corona.

    Baada ya viongozi wa G20 kufanya mkutano maalum kwa njia ya video kuhusu kukabiliana na virusi vya Corona, taarifa ya pamoja imetolewa na kusema kundi hilo limechukua hatua za haraka na zenye nguvu kusaidia uchumi na kulinda wafanyakazi na wafanyabiashara, haswa biashara ndogo ndogo na zenye ukubwa wa kati.

    Aidha taarifa imesema kuwa G20 itafanya kazi ili kuhakikisha upitaji wa kawaida wa mipaka kwa vifaa vya matibabu, bidhaa muhimu za kilimo na bidhaa nyingine na huduma, na kujitahidi kuondoa usumbufu kwa usambazaji wa huduma duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako