• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Shanghai Shenhua yataka Odion Ighalo arejee China kwa dau la paundi 400,000 kwa wiki

  (GMT+08:00) 2020-03-27 12:13:21

  Klabu ya Shanghai Shenhua ya hapa China imetoa ofa ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wake Odion Ighalo (30) ambaye anacheza kwa mkopo Manchester United. Mkataba wa sasa ulikuwa unamalizika mwaka 2022, lakini Shanghai baada ya kuridhika na kiwango chake cha hivi karibuni, wanataka kuendelea kummiliki Mnigeria huyo hadi mwaka 2024, kwa malipo ya paundi 400,000 kwa wiki. Kwa upande wake Ighalo anachusubiri ni ofa itakayotolewa na Man United baada ya mkopo wake kumalizika mwezi Juni mwaka huu kwani imekuwa ni ndoto yake ya maisha kukipiga kwa mashetani hao wekundu wa Jiji la Manchester.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako