• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Wachezaji wa FC Barcelona wakataa kukatwa mshahara kwa 70%

    (GMT+08:00) 2020-03-27 12:14:19

    Wachezaji wa FC Barcelona wapo katika mvutano mkubwa ndani kwa ndani na bodi ya timu yao kufuatia pendekezo la bodi hiyo la kutaka kuwakata mishahara. Rais wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu anaingia katika mvutano mzito na wachezaji hao kutokana na klabu kutaka kuwakata wachezaji hao kila mmoja asilimia 70 ya mshahara wake wakati huu Ligi ikiwa imesimama kwa sababu ya virusi vya corona.

    Bodi ya wakurugenzi jana ilifanya kikao kupitia video conference kujadili kuhusiana na makato hayo ya mishahara lakini kwa mujibu wa Diario Sport wachezaji hawajakubali makato ya asilimia 70. Hadi sasa Hispania inaripotiwa kuwa takribani jumla ya watu 4000 wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa virusi vya corona na klabu za soka zinakata mishahara ya wachezaji ili kupunguza hasara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako