• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Machinga watakiwa kuondoka barabarani

    (GMT+08:00) 2020-03-27 20:02:28
    Halamashauri ya Jiji la Dodoma imewataka wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara zao kwenye maeneo yasiyo rasmi ikiwamo barabarani, kuondoka kwa kuwa ni maeneo hatari kiusalama na kiafya.

    Ofisa Masoko wa Jiji hilo, James Yuna amesema maeneo kama barabara za magari na watembea kwa miguu, darajani na mitaroni ni hatari wafanyabiashara na wateja, hivyo wafanye biashara kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya biashara hizo badala ya kuvamia maeneo yasiyo rasmi kwao.

    Aliwataka viongozi wao kushirikiana na jiji kutoa elimu, ili kuondoa tatizo la kufanya biashara bila mpangilio wowote.

    Ofisa huyo pia aliwataka wafanyabiashara kufanya biashara kwenye masoko yaliyoko karibu kwenye kata zote kwa kuwa nafasi bado zinapatikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako