• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya Rais Xi kwenye mkutano wa kundi la nchi 20, yaonyesha mwelekeo wa mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-29 19:18:31

    Hotuba iliyotolewa na Rais Xi Jinping kwenye mkutano usio wa kawaida wa kundi la nchi 20 (G20) imesisitiza mwitikio wa pamoja kwenye tishio la pamoja la virusi vya Corona (COVID-19), na kuweka mwelekeo wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

    Kwenye mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video, Rais Xi alitoa mapendekezo manne ya nchi zote kuwa na dhamira kamili ya kupambana kwa pamoja dhidi ya ugonjwa huo, kuwa na mwitikio wa pamoja wa kudhibiti na kutibu ugonjwa huo katika ngazi ya kimataifa, na kuyaunga mkono mashirika ya kimataifa kutoa mchango halisi na kudumisha uratibu wa sera kuu za kiuchumi怂Wataalam kadhaa wamepongeza hotuba hiyo.

    Profesa Alan Barrell wa Chuo Kikuu cha Cambridge amesema hotuba ya Rais Xi imetoa mwito wa kuchukua hatua za pamoja dhidi ya changamoto kubwa wakati wa shinikizo na hatari inayowakabili watu duniani. Bw. Willian Jones wa jarida la habari za kijasusi kituo cha Washington, amesema hotuba ya Rais Xi ni hatua kuelekea upande sahihi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako