• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Alex Song kuishtaki timu yake kwa FIFA

    (GMT+08:00) 2020-03-30 08:22:22

    Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Arsenal, Alex Song anakusudia kuchukua hatua za kisheria na kuwafikisha mabosi wake wa sasa FC Sion mbele ya Shirikisho la Mpira wa Miguu duniania (FIFA) baada timu hiyo ya Uswizi kuamua kumtimua nyota huyo kutokana na kukataa kupunguziwa mshahara kipindi hiki ambacho michezo imesimamishwa ili kupambana na Virusi vya Corona. Song na baadhi ya wachezaji wengine wanane akiwemo na aliyekuwa nyota wa Arsenal, Johan Djourou wameondolewa ndani ya klabu hiyo kwa kile kinachodaiwa kushindwa kujibu ujumbe wa WhatsApp uliotumwa na rais wa timu hiyo Christian Constantin au kukataa ofa hiyo waliyoambiwa ya kupunguziwa mishahara yao ili kuiwezesha klabu hiyo kupambana na hali ya kiuchumi iliyosababishwa na kusimama kwa michezo kufuatia janga la Corona. Constantin aliwataka wachezaji kupunguziwa £10,750 kwenye mishahara yao ili kuiwezesha klabu hiyo ambayo inapitia kipindi kigumu cha uchumi kufuatia kufungwa kwa msimu wa ligi. Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Song mwenye umri wa miaka 32 amekiambia chombo cha habari cha RMC Sport kuwa Mwanasheria wake alishukhulikia swala hilo FIFA katika kuhakikisha anapata haki zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako