• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Anthony Yarde awata wakae ndani baada ya baba yake kufariki kwa virusi vya corona

    (GMT+08:00) 2020-03-30 08:22:45

    Mwanamasumbwi wa Uingereza Anthony Yarde amewataka watu wakae nyumbani baada ya baba yake kufariki kwa virusi vya corona. Mwanasumbwi huyo mwenye miaka 28 wa uzito wa juu amesema baba yake alikuwa mzima wa afya kabla ya kupata virusi. Amesema bado ana mshtuko lakini anatarajia hii itasaidia watu kukaa ndani. Na kusisitiza kuwa kadiri watu watakavyotoka nje ndio karantini itadumu kwa muda mrefu na ugonjwa kusambaa zaidi. Promota wa Yarde, Frank Warren, amesema anatarajia kuwa mashabiki wa Yarde watamsikiliza na kufuata ushauri wa serikali ili kuweza kupunguza taabu hii. Pambano linalofuata la Yarde lilipangwa kufanyika Aprili 11 dhidi ya Muingereza Lyndon Arthur, lakini limeahirishwa hadi Julai 11 kwasababu ya mlipuko wa corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako