• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya COVID-19 duniani yazaidi laki 7

    (GMT+08:00) 2020-03-30 09:31:28

    Takwimu mpya kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani zinaonyesha kuwa hadi kufikia saa 12 na dakika 45 GMT, idadi ya jumla ya maambukizi ya virusi vya Corona kote duniani imezidi laki 7.

    Takwimu zinaonyesha kuwa, Marekani ina idadi kubwa zaidi ya maambukizi duniani, ambayo imefikia laki 1.32, huku Italia ikiripoti vifo zaidi elfu 10 na kuwa nchi yenye vifo vingi zaidi vinavyotokana na virusi vya Corona.

    Mapema ya siku hiyo, Shirika la afya duniani WHO lilitangaza kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona imefikia 616,742. Takwimu kutoka WHO inaonyesha kuwa mpaka saa 10 mchana GMT idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona duniani ilikuwa imefikia 30,105.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako