• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona nchini Italia yapungua

    (GMT+08:00) 2020-03-30 10:06:05

    Ofisa wa afya wa Italia amesema, idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona vimepungua kwa siku mbili mfululizo, wakati huohuo idadi ya wagonjwa mahututi haijaongezeka.

    Tangu mlipuko wa virusi vya Corona uanze nchini Italia, Jumapili imeashiria mara ya tatu ambayo idadi ya vifo inapungua kwa siku mbili mfululizo, ingawa mwelekeo huo haujadumu kwa siku ya tatu.

    Jumapili vifo wa watu 756 viliripotiwa, idadi ambayo imepungua kutoka 899 ya Jumamosi, na 969 ya Ijumaa. Idadi ya vifo ya Ijumaa ilikuwa kubwa zaidi tangu mlipuko wa virusi hivyo uibuke nchini humo Februari 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako