• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Poulsen anamfuata Samatta Ligi Kuu England

  (GMT+08:00) 2020-03-30 16:47:31

  Mshambuliaji wa timu ya RB Leipzig ya Ujerumani, Yussuf Poulsen mwenye asili ya Tanzania ameripotiwa kuwindwa na klabu ya New Castle United inayoshiriki Ligi Kuu England, ikiwa ni mpango wa kuongeza makali kwenye safu yao ya ushambuliaji. Habari zinasema New Castle wako kwenye nafasi nzuri ya kumsajili nyota huyo ambaye amepoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha RB Leipzig. Poulsen alijiunga na timu hiyo Julai mwaka 2013 akitokea Lyngby BK ya Denmark ambako alisajiliwa kwa ada ya Euro milioni 1.55, na mkataba wake huo unatarajiwa kumalizika 2022. Msimu huu, Poulsen amefunga mabao matatu na kusaidia mabao matano katika michezo 20 aliyoichezea timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga. Kama akifanikiwa kwenda Uingereza, ataungana na Mtanzania Mbwana Samatta anayecheza Ligi Kuu England akiwa na timu ya Aston Villa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako