• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nia ya rais wa Marekani kutenganisha Marekani na China yaleta matokeo mabaya

  (GMT+08:00) 2020-03-30 19:49:07

  Jarida la the Atlantic la Marekani limechapisha makala iliyoandikwa na Profesa Peter Beinart wa Chuo Kikuu cha Mji wa New York, ikisema kitendo cha rais Donald Trump wa Marekani kutenganisha nchi yake na China kimeleta matokeo mabaya.

  Makala hiyo inasema, wakati Marekani inakabiliwa na hali mbaya ya maambukizi ya virusi vya Corona, ushirikiano kati yake na China ni muhimu sana, kwani China imefanikiwa kudhibiti virusi hivyo, na Marekani inapaswa kujifunza uzoefu wake. Hivi sasa China inapeleka vifaa vingi vya matibabu na kukinga virusi kwa nchi za Ulaya, ambavyo pia vinahitajika sana na Marekani. Wakati virusi vya Corona vinaenea kwa kasi duniani, China itakuwa kiwanda cha silaha dhidi ya virusi hivyo.

  Malaka hiyo pia inasema, virusi vya Corona vimethibitisha ukweli unaokwenda kinyume na mawazo ya rais huyo wa Marekani, kwamba katika dunia hii ambayo nchi zinaungana, kuzidisha ushirikiano wa kimataifa haswa na China kutalinda usalama wa Wamarekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako