• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatuliza uchumi wa dunia kwa hatua halisi

  (GMT+08:00) 2020-03-30 19:53:42

  Rais Xi Jinping wa China jana alikagua bandari ya Zhoushan mkoani Zhejiang, ambayo inashika nafasi ya kwanza duniani kwa kupokea na kusafirisha mizigo, na wakati dunia ikikabiliwa na maambukizi ya virusi vya COrona, China imetoa ishara ya kujitahidi kulinda utulivu wa mnyororo wa ugavi duniani.

  Kwenye mkutano wa Kundi la Nchi 20 uliofanyika kwa njia ya video, rais Xi alisema China itaongeza utoaji wa malighafi ya dawa, bidhaa za matumizi ya kila siku, na vifaa vya kukinga virusi kwa soko la dunia.

  Hivi karibuni China imetuma timu za madaktari katika nchi zinazokumbwa zaidi na COVID-19. Takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO zinaonesha kuwa, hadi kufikia saa 6 usiku wa leo kwa saa za China, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona imefikia karibu laki 6.4, na nchi na sehemu 202 duniani zimeripoti maambukizi ya ugonjwa huo, na athari ya ugonjwa huo kwa uchumi wa dunia itaendelea kuongezeka.

  Kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alivyosema kwenye barua yake kwa mkutano wa Kundi la Nchi 20, huu ni wakati wa kushikamana badala ya kutengana. Kwa ajili ya maslahi ya binadamu wote, jamii ya kimataifa inahitaji ushirikiano wa karibu zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako