• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Xavier Hernandez afunguka kuwa yupo tayari kurudi kama Kocha Mkuu wa Barcelona

    (GMT+08:00) 2020-03-31 08:33:15

    Nyota wa Barcelona, Xavier Hernandez amefunguka kuwa yupo tayari kurudi ndani ya miamba hiyo ya soka ya Hispania kama Kocha Mkuu. Kiungo huyo wa zamani wa Nou Camp alipewa nafasi ya kurithi mikoba ya Ernesto Valverde hapo mwaka jana lakini hatimaye alikataa fursa hiyo. Lakini baadae Barcelona ilihamia kwa Quique Setien na kukiongoza kikosi hicho na kufanikiwa kuleta ushindani mkubwa dhidi ya Real Madrid ndani ya La Liga. Baada ya mchezo wa mpira wa miguu kusimama kwa muda kufuatia mapambano dhidi ya virusi vya Corona habari za Xavi kurejea Barcelona akitoka kuifundisha Al Sadd ya Qatar, zimeanza kushika kasi upya. Xavi aliliambia gazeti la Hispania la La Vanguardi anaweka wazi kuwa anataka kurudi Barcelona na amevutiwa sana. Barcelona ina mkataba na Quique Setien mpaka 2022, lakini Xavi amefungua milango kwa klabu yake kama watahitaji huduma yake ya kuifundisha miamba hiyo ya soka ya La Liga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako