• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CORONA: Wanariadha 12 wakamatwa Kenya kwa kukaidi amri ya serikali ya kujiepusha na mikusanyiko

  (GMT+08:00) 2020-03-31 08:34:07

  Wanariadha 12 jana walikamatwa huko Iten, kaunti ya Elgeyo-Marakwet, kwa kufanya mazoezi kwa vikundi wakikaidi amri ya serikali ya kujiepusha na mikusanyiko ya kijamii na shughuli za michezo. Wanariadha hao ambao 10 ni Wakenya na wageni wawili, walipelekwa kituo cha polisi cha Iten kabla ya Maofisa wa Riadha wa Kenya kuingilia kati. Hata hivyo maafisa hao wamekiri kuwa wanariadha wana makosa. Kocha Elkanah Ruto amesema tukio hilo linahatarisha maisha ya wanariadha pamoja na jamii kwa ujumla. Wiki iliyopuita Shirikisho la Riadha la Kenya liliamuru kambi zote za mazoezi nchini kufungwa na wanariadha wamelekezwa kujiweka mbali na mikusanyiko na kufanya mazoezi mtu mmoja mmoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako