• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Russia na Marekani wafanya mazungumzo kwa njia ya simu kuhusu COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-31 08:49:25

    Rais Vladimir Putin na mwenzake wa Marekani Donald Trump jana wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu kuhusu mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Taarifa kutoka tovuti ya rais wa Russia inasema, marais hao wamefuatilia mlipuko wa virusi vya Corona kote duniani, kufahamishana kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya virusi hivyo katika nchi yao. Pia wamejadili suala la kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Taarifa kutoka ikulu ya Marekani inasema marais hao wamejadili maendeleo mapya na hatua zilizochukuliwa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona. Pande mbili pia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano ndani ya kundi la G20, kuhimiza kwa pamoja ushirikiano wa kimataifa kushinda vita dhidi ya virusi vya Corona na kufufua uchumi wa Dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako