• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona nchini Italia yazidi laki 1

  (GMT+08:00) 2020-03-31 09:58:19

  Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na idara ya ulinzi wa raia ya Italia inayoshughulikia kazi ya kukabiliana na dharura ya taifa, hadi jana watu 11,591 wamefariki dunia nchini humo kutokana na virusi vya Corona, huku idadi ya watu walioambukizwa ikiongezeka hadi kufikia 101,739.

  Wakati huohuo idadi ya wagonjwa waliopona jana pia imeongezeka kwa kiwango cha juu zaidi na kufikia 1,590.

  Habari pia zinasema waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Roberto Speranza, amesema karantini ya virusi vya Corona iliyoanza kutekelezwa nchini humo Machi 10, itarefushwa hadi Aprili 12 siku 9 zaidi kuliko muda uliopangwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako