• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Samatta aizidi kupeta, Galatasaray wamtaka

  (GMT+08:00) 2020-03-31 18:11:49

  Nyota wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga Aston Villa ya Ligi Kuu England, Mbwana Samatta, huenda akatua Galatasaray ya Uturuki iliyoonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba. Hata hivyo, Galatasaray inafuatilia mwenendo wa Aston Villa na kwamba iwapo klabu hiyo itashuka daraja, watatumia mwanya huo kumtwaa Samatta. Samatta aliyejiunga na Aston Villa Januari mwaka huu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, amefunga mabao mawili na timu yake hiyo mpya katika mechi za Ligi Kuu England. Inasemekana kuwa Galatasaray walikuwa wakimwania Samatta katika kipindi cha dirisha dogo la usajili la Januari, lakini walipigwa kikumbo na Aston Villa, hivyo kwa sasa wanajipanga kumnasa usajili wa kiangazi. Miamba hiyo ya soka Uturuki, inaamini Villa watakuwa tayari kuwauza wachezaji wao iwapo wakali hao wa England watashuka daraja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako