• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kuacha kitendo cha kunyanyapaa China

    (GMT+08:00) 2020-03-31 20:03:53

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inamtaka mkurugenzi wa ofisi ya sera za biashara na viwanda ya ikulu ya Marekani Bw. Peter Navarro kuelewa zaidi mazungumzo yaliyofanyika ijumaa iliyopita kati ya viongozi wa China na Marekani, na kuacha kitendo cha kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kufanya zaidi mambo yatakayonufaisha watu wa nchi hizo mbili.

    Habari zinasema, Bw. Navarro alisema, China imechelewa kuripoti mlipuko wa ugonjwa huo kwa wiki 6.

    Bibi Hua amesema, ukweli ni kwamba China ilianza kuripoti hali ya maambukizi ya virusi hivyo kwa Shirika la Afya Duniani na nchi nyingine mbalimbali ikiwemo Marekani mwanzoni mwa Januari. Ameongeza kuwa lengo la Navarro ni kuharibu ushirikiano wa China na Marekani katika kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako