• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 19 wa kikosi cha Zimamoto wafariki katika ajali ya moto wa msituni mkoani Sichuan, China

    (GMT+08:00) 2020-03-31 20:05:08

    Askari 19 wa kikosi cha jeshi la Zimamoto wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya moto wa msituni uliotokea jana mkoani Sichuan, China.

    Kufuatia ajali hiyo, Rais Xi Jinping wa China ameagiza kazi za uokoaji zifanyike kwa njia ya kisayansi, na kuhakikisha usalama wa watu.

    Ajali hiyo imetokea katika msitu uliopo kijiji cha Ma'an tarafa ya Jingjiu, mji wa Xichang mkoani Sichuan, na wakati kazi ya kuzima moto huo ilipokuwa ikiendelea, upepo uliongezeka kwa ghafla.

    Rais Xi amesema wakati serikali za mitaa zinajitahidi kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona na kurudisha uzalishaji, pia zinatakiwa kuimarisha kazi za kukinga maafa ya kiasili, ukiwemo moto wa msituni, ili kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu.

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang pia ametoa maelekezo muhimu kuhusu ajali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako