• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Mtanzania Atiki Ally ainyemelea rikodi ya Hasheem Thabeet NBA

    (GMT+08:00) 2020-04-01 08:57:00
    Mchezaji chipukizi wa Tanzania, Atiki Ally amesema kuchaguliwa kwake kwenye timu ya kwanza ya wachezaji nyota wa vyuo nchini Canada kumemnyooshea ndoto ya kucheza Ligi ya Kikapu nchini Marekani (NBA). Atiki aliyepo nchini Canada kwa sasa akitokea Chuo cha Themes Valley District School Board, anafuata nyayo za mchezaji wa kwanza Mtanzania kusajiliwa NBA, Hasheem Thabeet anayeichezea Fort Wayne Mad Ants iliyopo Indiana nchini Marekani. Kwa kawaida wachezaji wanaofuzu katika hatua hiyo hujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kuchaguliwa na timu zinazoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), ambayo inasifika kwa kulipa fedha nyingi wachezaji wake. Ally amechaguliwa kwenye timu ya kwanza ya wachezaji nyota na National Preparatory Association (NPA) chini Canada, na taarifa kutoka nchini humo zimeeleza kuwa kuchaguliwa kwake kunatokana na uwezo mkubwa aliouonyesha kwa kila mchezo aliocheza.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako