• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ajax yavunja mkataba na mchezaji wake aliyejeruhiwa akiitumikia timu hiyo

  (GMT+08:00) 2020-04-01 08:58:10

  Klabu ya Ajax ya Uholanzi ikiwa ni wiki moja tu imepita toka nyota wao Abdelhak Nouri aanze kuchezesha baadhi ya viungo vyake toka apoteze fahamu kwa miaka miwili na miezi 9 imeripotiwa kuwa kusitisha mkataba na Nouri ambaye bado yupo kitandani katika majeraha ambayo aliyapata kwa kuanguka uwanjani akiitumikia timu hiyo katika mchezo wa kirafiki. Kwa sasa Ajax ambayo ilikuwa ikimlipa mshahara Nouri toka July 2017 kwa heshima ya kupata matatizo akiwa katika timu yao imepanga kukutana na wanasheria na familia ya mchezaji huyo. Nouri alianguka na kupoteza fahamu uwanjani Julai 2017 kwa tatizo la moyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Werder Bremen. Wiki moja iliyopita alizinduka na fahamu kumrejea baada ya kupoteza fahamu kwa miaka miwili na miezi 9, kwa mujibu wa kaka yake Nouri sasa anachezesha macho, kula na kuchezesha sura.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako